Mwendelezo wa mashambulizi ya Marekani na Uingereza Yemen Magharibi
(last modified Thu, 24 Oct 2024 07:43:25 GMT )
Oct 24, 2024 07:43 UTC
  • Mwendelezo wa mashambulizi ya Marekani na Uingereza Yemen Magharibi

Ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi mengine makubwa huko Yemen Magharibi.

Kanali ya Sahab imelinukuu shirika la habari la  IRNA, kwamba ndege za kivita za Marekani na Uingereza zimefanya mara mbili mashambulizi makali ya mabomu katika uwanja wa ndege wa Al Hudaydah ulioko magharibi mwa Yemen.

Kufikia sasa, hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu hasara wala maafa yaliyotokana na shambulio hilo.

Katika miezi michache iliyopita, maeneo tofauti ya Yemen hususan mkoa wa Al Hudaydah  yamekuwa yakilengwa na kushambuliwa vikali na ndege za kivita za Marekani na Uingereza.

Mashambulio hayo ya Marekani na Uingereza yametekelezwa baada ya jeshi la Yemen kulenga katika miezi iliyopita meli za utawala wa Kizayuni au zile zinazoelekea katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel, katika Bahari Nyekundu na mlango wa bahari wa Bab al-Mandab, ili kuunga mkono muqawama wa wananchi wa Palestina wanaodhulimiwa huko Ukanda wa Gaza.

Tangu kuanza kwa vita vya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, jeshi la Yemen limekuwa likijitolea kuunga mkono muqawama wa wananchi wa Palestina kwa kuendesha mashambulio dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na kuapa kuwa utaendeleza mashambulizi hayo hadi pale utawala huo bandia utakaposimamisha mashambulizi hayo ya kikatili dhidi ya wakazi wa  Gaza.

Tags