Trump aituhumu UK kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani
(last modified Thu, 24 Oct 2024 02:18:29 GMT )
Oct 24, 2024 02:18 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Mgombea wa urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump amewasilisha malalamiko yake kuhusu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani unaofanywa na chama tawala nchini Uingereza.

Maafisa wa Chama cha Leba wameripotiwa kuwashauri Wademocrats kuhusu mikakati, huku wanaharakati wao wakifanya kazi katika majimbo yenye ushindani mkubwa, lakini wanasisitiza kwamba yote haya ni halali kwa kuwa hawajatoa pesa yoyote kwa chama.

Katika malalamiko kwa Kamisheni ya Uchaguzi (FEC), timu ya kampeni ya Trump inaituhumu Leba kwa "uingiliaji wa wazi wa kigeni" katika uchaguzi wa Marekani, kwa njia ya "michango haramu" iliyokubaliwa na Democrats na mgombea wao, Makamu wa Rais Kamala Harris.

Faili hilo dhidi ya Chama cha Leba limenukuu kipengee cha sheria ya uchaguzi ya US kinachosema: Raia wa kigeni hawaruhusiwi kutoa "mchango wa pesa au kitu kingine cha thamani, au kutoa ahadi ya mchango," ili kuunga mkono mgombeaji wa Marekani, "moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja."

Miongoni mwa ushahidi uliotajwa na timu ya kampeni ya Trump ni ripoti ya Washington Post kwamba "wanamkakati wanaohusishwa na Chama cha Leba cha Uingereza wamekuwa wakitoa ushauri kwa Kamala Harris kuhusu jinsi ya kuwashawishi wapiga kura waliokata tamaa na kuendesha kampeni itakayowahakikishia ushindi.

Tags