Ripoti: Netanyahu na Gallant wamekimbilia kwenye mahandaki
(last modified Sat, 26 Oct 2024 11:01:35 GMT )
Oct 26, 2024 11:01 UTC
  • Ripoti: Netanyahu na Gallant wamekimbilia kwenye mahandaki

Gazeti moja la utawala wa Kizayuni limeripoti kuwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu na Yoav Gallant Waziri wa Vita wa utawala huo wamekimbilia katika mahandaki kujificha kwa kuhofia kushambuliwa.

Wakati huo huo taarifa mbalimbali za vyombo vya habari zimearifu kuwa, Netanyahu na Gallant leo wamekimbilia mahandakini wakihofia mashambulizi ya wanamuqawama. 

Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant wameripotiwa kukimbilia mahandakini baada ya Israel kuvishambulai baadhi ya vituo vya kijeshi hapa Tehran, katika mji wa kati wa Ilam na huko Khuzestan, kusini magharibi mwa Iran.

Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Kamandi ya Ulinzi wa Anga ya Iran imetoa taarifa na kubainisha kuwa mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mdogo na kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi umefanikiwa kuzuia na kuzima kitendo hicho cha uchokozi.

Mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Chokochoko hizo zimetokea licha ya Iran kutahadharisha kuhusu hatua za uchokozi wa Israel.

Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Kamandi ya Ulinzi wa Anga ya Iran pia imewataka wananchi kusalia watulivu, kudumisha mshikamano na kutegemea taarifa zinazotangazwa na shirika la habari la taifa. Aidha taarifa hiyo imewatolea wito wananchi wa Iran kupuuza taarifa za uwongo za vyombo vya habari vya adui. 

 

Tags