Makumi wauawa na kujeruhiwa na Saudia huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11815-makumi_wauawa_na_kujeruhiwa_na_saudia_huko_yemen
Makumi ya raia wa Yemen wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia katika maeneo mbalimbali ya Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2016 02:55 UTC
  • Makumi wauawa na kujeruhiwa na Saudia huko Yemen

Makumi ya raia wa Yemen wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia katika maeneo mbalimbali ya Yemen.

Ndege za kivita za Saudi Arabia zimeshambulia maeneo mbalimbali ya Yemen mara 75 na kuua makumi ya raia na kujeruhi wengine kadhaa. 

Ndege za kivita za utawala vamizi wa Saudia zimeshambulia maeneo mbalimbali ya wilaya ya al Qataf katika mkoa wa Sa'ada na kuuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili. Raia wawili wengine wameuawa katika mashambulizi ya wanajeshi wa Saudia katika mkoa wa al Jauf. 

 

Ndege za kivita za Saudia zashambulia mara 75 maeneo mbalimbali ya Yemen

Ndege vamizi za Saudi Arabia zimezishambulia mara kadhaa wilaya za Nahm katika mkoa wa San'aa, Dhabab katika mkoa wa kusini wa Ta'iz na kuushambulia pia mkoa wa al Hajjah; mashambulizi yaliyosababisha vifo na kujeruhi raia kadhaa wa Yemen. 

Hii ni katika hali ambayo wanajeshi wa Saudia wamezidisha mzingiro katika wilaya ya al Sarar huko Ta'iz Yemen. Wakazi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la chakula na madawa baada ya vikosi hivyo vamizi kuzuia kuingizwa bidhaa hizo za msingi katika eneo hilo.