Wanahabari Waislamu waungana na mwandishi mateka wa Mpalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1201-wanahabari_waislamu_waungana_na_mwandishi_mateka_wa_mpalestina
Jumuiya ya Waandishi Habari Waislamu imetangaza mshikamano wake na mwandishi habari mateka wa Palestina anayeshikiliwa katika korokoro za utawala ghasibu wa Israel, Muhammad al Qiq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 13, 2016 22:26 UTC
  • Wanahabari Waislamu waungana na mwandishi mateka wa Mpalestina

Jumuiya ya Waandishi Habari Waislamu imetangaza mshikamano wake na mwandishi habari mateka wa Palestina anayeshikiliwa katika korokoro za utawala ghasibu wa Israel, Muhammad al Qiq.

Jumuiya ya Waandishi Habari Waislamu imelaani vikali jinai zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Muhammad al Aqiq, mwandishi habari wa Palestina anayefanya mgomo wa kula akipinga ukatili na unyama wa Israel na kutangaza kuwa, Wazayuni wamezidisha ukatili na unyama wao dhidi ya taifa la Palestina kutokana na kukosekana idara ya kweli ya nchi za Magharibi na jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israel huko Palestina.

Taarifa ya Jumuiya ya Waandishi Habari Waislamu imezitaka jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu kufanya jitihada zaidi za komesha jinai na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumuiya hiyo pia imeitaka jamii ya waandishi habari na wamiliki wa vyombo vya habari kutekeleza wadhifa wao wa kumtetea mwandishi huyo wa habari anayeshikiliwa mateka na wasiuruhusu utawala haramu wa Israel kutimiza ukatili wake chini ya mwavuli wa kimya cha nchi zinazodai kutetea demokrasia na haki za binadamu.

Muhammad al Qiq, mwandishi habari wa Palestina anayeshikiliwa katika korokoro za Israel alianza mgomo wa kula siku 80 zilizopita akipinga kukamatwa kwake bila na makosa yoyote. Madaktari wanasema hali ya mwandishi huyo wa habari wa Palestina ni mbaya sana.