Beki Mfaransa wa Klabu ya Barcelona ataka kukombolewa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141508-beki_mfaransa_wa_klabu_ya_barcelona_ataka_kukombolewa_palestina
Jules Koundé, beki Mfaransa wa klabu ya soka ya Barcelona ya Uhispania, kwa mara nyingine ameonyesha himaya na uungaji mkono wake kwa taifa la Palestina na kutoa wito wa kukombolewa ardhi hiyo.
(last modified 2026-09-17T02:46:55+00:00 )
Sep 17, 2026 02:44 UTC
  • Beki Mfaransa wa Klabu ya Barcelona ataka kukombolewa Palestina

Jules Koundé, beki Mfaransa wa klabu ya soka ya Barcelona ya Uhispania, kwa mara nyingine ameonyesha himaya na uungaji mkono wake kwa taifa la Palestina na kutoa wito wa kukombolewa ardhi hiyo.

Jules Koundé, beki Mfaransa wa klabu ya Barcelona, amevuta hisia za vyombo vya habari vya michezo na mitandao ya kijamii baada ya kushiriki tena (repost) ujumbe mkali na wenye maana nzito kutoka kwa mwanamuziki wa rap wa Marekani, Macklemore.

Macklemore alikuwa amechapisha awali ujumbe huo akizungumzia madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msimamo wake wa kisiasa wa kuunga mkono Palestina, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa baadhi ya maonesho yake kufutwa.

Macklemore aliandika:

“Ikomboeni Palestina. Lakini ikiwa maneno haya yatanigharimu nafasi ya kutumbuiza jukwaani, huku yakiwa yamesaidia kufungua tena njia ya mazungumzo kuhusu Palestina, basi hii ndiyo safari yenye mafanikio makubwa zaidi ambayo nimewahi kushiriki.”

Mchezaji wa Ufaransa Jules Koundé, anayekipiga katika klabu ya Barcelona, huku nyuma pia amewahi kutuma ujumbe kwa wafuasi wake kuhusu hali inayoendelea Palestina. Katika ujumbe huo aliandika: “Chukueni muda kusoma ujumbe na kusikiliza video nzima kabla ya kujibu na kutoa hukumu za haraka, kwa sababu jambo hili ni muhimu sana.”

“Katika soka la Ulaya na kwingineko, baadhi ya nyota wameendelea kutumia majukwaa yao kueleza mshikamano wao na wananchi wa Palestina. Miongoni mwao ni Mohamed Salah, Paul Pogba, Riyad Mahrez, Sadio Mané, Karim Benzema na Jules Koundé, ambao kwa nyakati tofauti wametoa jumbe za kuunga mkono Palestina au kulaani mauaji na ukatili dhidi ya raia.”

Mnamo Januari 2026, katika hafla ya hisani mjini Barcelona iliyolenga kuwaunga mkono Wapalestina, Pep Guardiola aliyekuwa mkufunzi wa Manchester City alisema kuwa watoto wa Palestina “wameachwa peke yao na wametelekezwa,” na akatoa wito kwa watu kutokupuuza mateso yao.