Saudia yadai haijaiwekea mzingiro Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i12310-saudia_yadai_haijaiwekea_mzingiro_yemen
Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unaendeleza mzingiro wa ardhini, baharini na angani dhidi ya Yemen umedai kuwa haujaizingira nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2016 00:01 UTC
  • Saudia yadai haijaiwekea mzingiro Yemen

Muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unaendeleza mzingiro wa ardhini, baharini na angani dhidi ya Yemen umedai kuwa haujaizingira nchi hiyo ya Kiarabu.

Muungano huo vamizi wa nchi kadhaa za Kiarabu umetoa taarifa na kutangaza kuwa unaruhusu kuingizwa nchini Yemen misaada ya kibinadamu, bidhaa za biashara na bidhaa zinazotokana na mafuta baada ya kuzifanyia ukaguzi.

Taarifa ya muungano huo wa kijeshi unaoongozwa na Saudia imedai kuwa muungano huo haujaiwekea mzingiro Yemen bali unatekeleza maazimio ya kimataifa ya kuzuia uingizaji silaha kimagendo nchini humo.

Mashambulio ya anga ya Saudia dhidi ya Yemen

Muungano vamizi wa kijeshi ambao umeizingira Yemen kutokea angani, baharini na nchi kavu huziruhusu meli kuelekea bandari za nchi hiyo baada ya kuzikagua shehena za meli hizo kwenye bandari za Saudia au Djibouti.

Madai ya Saudia ya kutoiwezeka mzingiro Yemen yanatolewa katika hali ambayo kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu nchini Yemen kumeufanya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh uwe kwenye mashinikizo ya kuutaka uhitimishe mzingiro dhidi ya nchi hiyo.

Ni karibu mwaka mmoja na nusu sasa Saudia ikishirkiana na muungano wake bandia wa kijeshi imeizingira na kuishambulia Yemen kutokea angani na ardhini kwa kisingizio cha kutaka kuirejesha ile utawala wa Aal Saud unayoiita serikali 'halali' ya Abd Rabbuh Mansur Hadi.

Abd Rabbuh Mansur Hadi, aliyejiuzulu urais na kuitoroka nchi

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo na taasisi nyingi za miundombinu ya nchi hiyo masikini zimeteketezwa bila ya watawala wa Aal Saudi kufikia malengo yao yasiyo ya kibinadamu.../