Jinai ya kutisha; Israel yaua shahidi Wapalestina 150 Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128262-jinai_ya_kutisha_israel_yaua_shahidi_wapalestina_150_gaza
Wapalestina zaidi ya 150 wameuawa shahidi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, huku eneo hilo la pwani likishuhudia siku yake mbaya zaidi tangu mwezi Mei, wakati utawala wa Israel uliposhadidisha mauaji yake ya kimbari dhidi ya eneo hilo.
(last modified 2025-07-13T02:17:07+00:00 )
Jul 13, 2025 02:02 UTC
  • Jinai ya kutisha; Israel yaua shahidi Wapalestina 150 Gaza

Wapalestina zaidi ya 150 wameuawa shahidi katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, huku eneo hilo la pwani likishuhudia siku yake mbaya zaidi tangu mwezi Mei, wakati utawala wa Israel uliposhadidisha mauaji yake ya kimbari dhidi ya eneo hilo.

Mauaji hayo ya kutisha yalifanywa na wanajeshi makatili wa Kizayuni jana Jumamosi, ambapo Wapalestina 34 waliuawa shahidi kutokana na uvamizi wa Israel uliowalenga walipokuwa wakisubiri msaada wa kibinadamu.

Aidha jana Jumamosi ilishuhudia jeshi la Israel likifanya mauaji mengi makubwa, abayo yalilenga maeneo ya makazi ya raia. Vyombo vya habari vya Muqawama vilisimulia baadhi ya matukio ya kutisha ya jana, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mabaya katika mji wa Jabalia Al-Nazla kaskazini mwa Gaza.

Mashambulizi hayo yalilenga nyumba zisizopungua tano, na kuzika takriban watu 20 wa familia mbili chini ya vifusi. Muda mfupi baadaye, shambulio la ndege zisizo na rubani lililenga mkusanyiko wa raia katika Kambi ya Wakimbizi ya al-Shati, ambayo vile vile iko kaskazini mwa Gaza, na kusababisha mauaji mengine ya watu wanane, ambao miili yao ilichanika vipande vipande.

Vikosi vya Israel pia vilifyatua "mkanda wa moto" mkubwa kwenye mji wa Beit Hanoun, kwenye ukingo wa kaskazini mashariki mwa Gaza, huku pia wakiendelea na kampeni yao ya kuvurumisha makombora na kubomoa makazi katika mji wa kusini wa Khan Younis.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari  vya Israel dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, watu karibu 58,000 wameuawa shahidi na wengine 137,800, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.