Jeshi la Israel limeiba punda wa Ghaza na kuwasafirisha kuwapeleka Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128366-jeshi_la_israel_limeiba_punda_wa_ghaza_na_kuwasafirisha_kuwapeleka_ufaransa
Jeshi la utawala kizayuni wa Israel limeripotiwa kuiba mamia ya punda kutoka Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro, kuwavusha kimagendo hadi Israel, na kisha kuwasafirisha kuelekea Ufaransa ili kuzuia wasitumike katika ujenzi upya wa Ghaza.
(last modified 2026-01-24T06:04:10+00:00 )
Jul 15, 2025 15:44 UTC
  • Jeshi la Israel limeiba punda wa Ghaza na kuwasafirisha kuwapeleka Ufaransa

Jeshi la utawala kizayuni wa Israel limeripotiwa kuiba mamia ya punda kutoka Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro, kuwavusha kimagendo hadi Israel, na kisha kuwasafirisha kuelekea Ufaransa ili kuzuia wasitumike katika ujenzi upya wa Ghaza.

Hayo yameripotiwa na chaneli ya Israel ya Kan ambayo imebainisha kuwa, uporaji huo wa makumi ya punda kutoka Ukanda wa Ghaza umefanywa kwa uratibu na mashirika ya utawala wa kizayuni na kwa ushirikiano wa taasisi za Ulaya, hususan kutoka nchi za Ufaransa na Ubelgiji.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel wamepora punda haoa katika maeneo waliyovamia ndani ya Ukanda wa Ghaza, kwa kisingizio cha "kuwaokoa na magonjwa na eti kutokana na kupuuzwa".

Vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel vimeuripoti uporaji huo kuwa eti ni "operesheni ya uokoaji wa mifugo," na kupuuza kueleza ukweli kwamba wamiliki wake Wapalestina waliwategemea wanyama hao kama njia muhimu ya usafirishaji ili kujinusuru na mashambulizi ya kinyama na mauaji ya kimbari yaayofanywa na utawala wa kizayuni huko Ghaza.

Chini ya sheria za kimataifa, unyakuzi unaofanywa kwa nguvu wa mali za kiraia wakati wa vita unatambuliwa kama uhalifu wa kivita.

Ripoti ya Kan imefichua pia kwamba punda walioibiwa kutoka Ghaza walihamishiwa kwenye shamba la Israel linaloitwa "Starting Over Sanctuary" huko Moshav Harot, kusini mwa Tel Aviv, linaloendeshwa na mzayuni aitwaye Sharon Cohen.

Kwa mujibu wa chaneli hiyo ya Israel, mnamo tarehe 18 Mei 2025, shehena ya kwanza ya punda 58 iliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion kuelekea Uwanja wa Ndege wa Liège nchini Ubelgiji, na kisha kupelekwa kwenye mazizi ya wanyama yaliyoko nchini Ufaransa na Ubelgiji.../