Ansarullah yapiga kwa kombora, droni maeneo hasasi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128420-ansarullah_yapiga_kwa_kombora_droni_maeneo_hasasi_ya_israel
Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen vimeshambulia maeneo matatu nyeti ya Israel kwa kombora la balestiki na ndege nne zisizo na rubani, baada ya kuulazimisha utawala huo ghasibu kutangaza kufungwa kwa moja ya bandari zake muhimu.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jul 17, 2025 01:09 UTC
  • Ansarullah yapiga kwa kombora, droni maeneo hasasi ya Israel

Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen vimeshambulia maeneo matatu nyeti ya Israel kwa kombora la balestiki na ndege nne zisizo na rubani, baada ya kuulazimisha utawala huo ghasibu kutangaza kufungwa kwa moja ya bandari zake muhimu.

Wanajeshi hao walitangaza kufanya operesheni hizo katika taarifa ya jana Jumatano, na kubainisha kuwa maeneo yaliyolengwa ni angatua ya Ben Gurion, uwanja wa ndege muhimu zaidi kwa utawala wa Israel, kituo cha kijeshi cha Israel katika jangwa la Negev, na bandari pekee ya utawala huo katika Bahari Nyekundu, ulioko katika mji wa Eilat unaokaliwa kwa mabavu.

Akitoa taarifa hiyo, Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema operesheni ya kwanza ilipiga uwanja wa ndege wa Ben Gurion kwa kombora la balestiki la Zulfiqar.

Shambulio hilo limesababisha athari nyingi hasi, na kulazimisha "mamilioni" ya walowezi haramu wa utawala huo pandikizi kutafuta makazi mbadala, ameongeza Brigedia Jenerali Yahya Saree.

Operesheni zilizofuata za wanamuqawama wa Ansarullah zililenga uwanja wa ndege, kituo cha kijeshi, na bandari, kwa kutumia droni nne za kubebea mabomu, afisa huyo wa vikosi vya Yemen amesema.

Wakati huo huo, Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ya Yemen imelaani vikali mashambulizi ya anga ya jana Jumatano ya Israel dhidi ya Syria, na kueleza kuwa hu ni "uchokozi wa kikatili wa Wazayuni" na "ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Syria".

Imesema mashambulio hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuvuruga uthabiti wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, na kupanua ushawishi wa Israel katika eneo la Asia Magharibi.