Brigedi za al Qassam zashambulia makao makuu ya jeshi la Israel
Brigedi za Izzudin Qassam, ambalo ni tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) zimetangaza kuwa zimeshambulia kwa roketi makao makuu ya jeshi la Israel.
Tawi hilo la kijeshi la harakati ya Hamas limetangaza katika taarifa yake ya leo Jumatano kwamba limeshambulia makao makuu ya jeshi la utawala wa Kizayuni kusini magharibi mwa mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Brigedi za Izzuddin Qassam zimetangaza kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa roketi ya masafa mafupi ya Rajum ya milimita 114.
Brigedi za al Qassam kabla ya kutekeleza shambulizi hili la leo, zilitangaza kuangamiza kifaru cha utawala wa Kizayuni katika eneo la Jafrawi kusini mashariki kwa Dei al Balah huko katikati mwa Ukanda wa Gaza kwa kutumia roketi ya al Yasin 105.
Tangu kuanza vita katika Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023 baada ya wanamapambano wa Palestina kutekeleza Operesheni kubwa ya "Al-Aqsa "; jeshi la Israel limekabiliwa na mfululizo wa vipigo vizito na vilivyoligharimu pakubwa ambavyo vimeliaathiri pakubwa kisaikolojia na kistratijia.
Weledi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa muqawama wa Palestina licha ya gharama zote hizo umeweza kubadilisha milinganyo ya vita hivyo na kulitia mtegoni jeshi la Israel katika vita vya gharama kubwa na vya kiukatili ambapo hakuna matarajio ya wazi ya ushindi kwa wavamizi hao.