UEFA yamuenzi 'Pele wa Palestina' aliyeuliwa na jeshi la Israel Ghaza wakati anangojea chakula
Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA, umemuenzi nahodha na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Palestina Suleiman al-Obeid, ambaye aliuawa shahidi katika shambulizi la kinyama la utawala wa kizayuni wa Israel alipokuwa akisubiri msaada wa chakula huko Ghaza siku ya Jumatano.
"Kipaji ambacho kilitoa matumaini kwa watoto wengi, hata katika nyakati za giza," imeeleza UEFA katika andiko ililoweka kwenye mtandao wa kijamii.
Chama cha Soka cha Palestina (PFA) kimetangaza kuwa al-Obeid, aliyeuawa shahidi akiwa na umri wa miaka 41, ameacha kizuka na watoto wawili wa kiume na watatu wa kike.
UEFA imeendelea kumuelezea al-Obeid: "Swala, Lulu Nyeusi, Henry wa Palestina, na Pele wa soka ya Palestina, zote hizo ni lakabu za nyota huyo aliyepitia kwenye viwanja vya kuchezea soka vya Palestina" .

PFA imeeleza pia kwamba, idadi ya wanachama wa chama hicho waliouawa huko Ghaza kutokana na mashambulio ya kinyama ya jeshi la Kizayuni hadi sasa imefikia 321, wakiwemo wachezaji, makocha wa timu, wasimamizi, waamuzi na wajumbe wa bodi za klabu.../