Askari watano wa Kizayuni watiwa mbaroni kwa kuiba silaha
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i13207-askari_watano_wa_kizayuni_watiwa_mbaroni_kwa_kuiba_silaha
Askari kadhaa wa utawala haramu wa Israel wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuiba silaha huko katika ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 14, 2016 03:04 UTC
  • Askari watano wa Kizayuni watiwa mbaroni kwa kuiba silaha

Askari kadhaa wa utawala haramu wa Israel wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuiba silaha huko katika ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Taarifa kutoka Israel zimeripoti kuwa, askari hao watano walitiwa mbaroni jana Jumamosi na polisi ya utawala huo kwa tuhuma za kuiba maroketi 13 na mabomu 77 kutoka kambi ya jeshi huko kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Askari wa Israel akiwa hajui hatma yake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu

Hadi sasa vyombo vya usalama wa jeshi la utawala huo haramu havijafanikiwa kunasa silaha zilizoibwa na askari hao. Polisi ya Israel imetangaza kuwa, inaendelea kukusanya nyaraka na ushahidi dhidi ya askari hao waliotiwa mbaroni.

Wiki iliyopita pia polisi ya utawala ghasibu wa Israel ilimtia mbaroni askari mwingine kwa kujihusisha na vitendo vya ununuzi na uuzaji silaha na zana za jeshi kutoka maghala ya jeshi hilo huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Baadhi ya askari wa Israel wanaotuhumiwa kuiba silaha

Miezi kadhaa iliyopita vyombo vya utawala wa Kizayuni viliripoti ongezeko la vitendo vya wizi wa silaha kutoka maghala yake ya kijeshi. Inafaa kufahamika kwamba utawala huo bandia unakabiliwa na matatizo chungu nzima ikiwemo ya ufisadi wa maafisa wa jeshi na pia kukimbia idadi kubwa ya vijana kutoka jeshini.