Saudia yashambulia hospitali Yemen; yaua raia 25 na kujeruhi 20
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i13342-saudia_yashambulia_hospitali_yemen_yaua_raia_25_na_kujeruhi_20
Raia wasiopungua 25 wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulio la anga la ndege za utawala vamizi wa Saudi Arabia dhidi ya hospitali moja kaskazini mwa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 15, 2016 23:17 UTC
  • Saudia yashambulia hospitali Yemen; yaua raia 25 na kujeruhi 20

Raia wasiopungua 25 wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulio la anga la ndege za utawala vamizi wa Saudi Arabia dhidi ya hospitali moja kaskazini mwa Yemen.

Shambulio hilo ambalo ni muendelezo wa ukiukaji makubaliano ya usitishaji vita unaofanywa na Saudia lilifanywa jana na kulenga hospitali moja katika mji wa Abs mkoani Hajjah.

Ripoti zinaeleza kuwa magari ya kubebea wagonjwa yalielekea haraka kwenye eneo la tukio kuwasaidia majeruhi.

Kanali ya televisheni ya al-Masirah ya Yemen imeripoti kuwa wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwemo madaktari na wauguzi pamoja na watoto ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la kinyama la Saudia.

Maiti ya mtu aliyeuawa katika shambulio la Saudia dhidi ya hospitali jana 

Shirika la Madkatari Wasio na Mipaka (MSF) limethibitisha kushambuliwa hospitali ya mji wa Abs ingawa halikutaja idadi rasmi ya watu waliouliwa na kujeruhiwa.

Msemaji wa shirika hilo Malak Shaher amesema shirika lao limekuwa na timu ya madaktari katika hospitali hiyo ya umma iliyoko kwenye mji wa pwani tangu mwaka uliopita wa 2015.

Shambulio la jana Jumatatu limefanywa baada ya masaa chini ya 48 tangu tangu MSF liliporipoti kuwa mashambulio ya anga ya Saudia yamelenga shule moja ya mkoa wa kaksazini wa Sa'ada na kuua watoto 10.

Mmoja wa watoto waliojeruhiwa katika shambulio dhidi ya shule mkoani Sa'ada

Kwa mujibu wa duru za harakati ya Ansarullah, mashambulio ya anga ya Saudia na washirika yanayofanywa dhidi ya Yemen bila ya idhini yoyote kimataifa yameshaua karibu watu10,000, wengi wao wakiwa ni raia.../