Iran kuwatibu waliojeruhiwa katika hujuma ya kinyama ya Saudia nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i17227-iran_kuwatibu_waliojeruhiwa_katika_hujuma_ya_kinyama_ya_saudia_nchini_yemen
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema iko tayari kuwapokea na kuwatibu waliojeruhiwa hivi karibuni katika hujuma ya kikatili ya ndege za kivita za Saudia dhidi ya watu waliokuwa wamekusanyika katika mazishi nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2016 23:58 UTC
  • Iran kuwatibu waliojeruhiwa katika hujuma ya kinyama ya Saudia nchini Yemen

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema iko tayari kuwapokea na kuwatibu waliojeruhiwa hivi karibuni katika hujuma ya kikatili ya ndege za kivita za Saudia dhidi ya watu waliokuwa wamekusanyika katika mazishi nchini Yemen.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran Iraj Harichi amesema, 'kwa kuzingatia jinai ya kinyama ya Saudia huko Sanaa mji mkuu wa Yemen ambapo idadi kubwa ya watu walijeruhiwa, Wizara ya Afya ya Iran inatangaza kuwa tayari kuwapokea majeruhi wa Yemen na kuwapa huduma bora zaidi ili kuokoa afya yao."

Aidha amesema  msaada huo unaweza kupunguza sehemu ya machungu na masaibu mengi walionayo watu wanaodhulumiwa nchini Yemen.

Jinai ya Saudia mjini Sanaa

Itakumbukwa kuwa, siku ya Jumamosi Alasiri, ndege za kivita za Saudi Arabia zilivamia kikao cha mazisihi kaskaziani mwa Sanaa mji mkuu wa Yemen ambapo watu zaidi ya 160 waliuawa na wengine zaidi ya 600 kujeruhiwa. Baadhi ya duru zinadokeza kuw aidaid ya waliopoteza maisha ni kubwa hasa kwa kuzingatia hali ya majeruhi wengi ilikuwa mahututi punde baada ya kujiri jinai hiyo ya kivita.