Syria: Jinai za magaidi zitakoma kwa kusimamishwa misaada wanayopata kutoka nje
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i19243-syria_jinai_za_magaidi_zitakoma_kwa_kusimamishwa_misaada_wanayopata_kutoka_nje
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema jinai za makundi ya kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo zitakoma pale tu utakapohitimishwa uungaji mkono na misaada kutoka nje inayotolewa kwa magaidi hao.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Nov 11, 2016 08:02 UTC
  • Syria: Jinai za magaidi zitakoma kwa kusimamishwa misaada wanayopata kutoka nje

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema jinai za makundi ya kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo zitakoma pale tu utakapohitimishwa uungaji mkono na misaada kutoka nje inayotolewa kwa magaidi hao.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeeleza hayo katika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kwa Baraza la Usalama la umoja huo na kubainisha kuwa jinai za makundi ya kigaidi dhidi ya raia, kuwatumia wananchi wa Syria kama ngao ya kibinadamu, kuandamwa na mashambulio mtawalia ya magaidi hao miji iliyozingirwa ya Foua na Kefraya na jinai za magaidi katika kitongoji cha Hadhr, yote hayo yanadhihirisha utambulisho na sura halisi za magaidi wa makundi hayo yanayosaidiwa na kuungwa mkono kifedha na kwa silaha na tawala za Saudi Arabia, Qatar na Uturuki na ambazo zinashajiishwa kufanya hivyo na baadhi ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh linaloungwa mkono na madola ya kigeni

Huku ikiashiria kuwa miji miwili ya Foua na Kefraya imezingirwa na magaidi wa kundi la Jaishul-Fat'h kwa muda wa miaka miwili sasa na misaada ya chakula ya Umoja wa Mataifa imeshindwa kufikishwa katika miji hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imebainisha kuwa nchi wanachama wa kudumu na wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hazijali wala kuzipa umuhimu wowote jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi nchini Syria.../