Palestina; elekeo la macho ya jamii ya kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i21910-palestina_elekeo_la_macho_ya_jamii_ya_kimataifa
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), Ahmad Abul Ghaith na Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza kuwa kadhia ya Palestina inaendelea kuwa suala la msingi la kushughulikiwa kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 22, 2016 04:19 UTC
  • Palestina; elekeo la macho ya jamii ya kimataifa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), Ahmad Abul Ghaith na Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza kuwa kadhia ya Palestina inaendelea kuwa suala la msingi la kushughulikiwa kimataifa.

Wawili hao walitoa sisitizo hilo siku ya Jumanne katika kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Umoja wa Ulaya kilichofanyika mjini Cairo, Misri makao makuu ya Arab League.

Akizungumza mwanzoni mwa kikao hicho, Abul Ghaith alisema, eneo la Mashariki ya Kati na Ulimwengu wa Kiarabu zinapita katika kipindi nyeti na hasasi. Mbali na kutilia mkazo tena ulazima wa kupambana na ugaidi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu alisema, licha ya kuendelea migogoro kadhaa katika eneo, kadhia ya Palestina ingali ndilo suala kuu na kipaumbele cha kwanza kwa Ulimwengu wa Waarabu.

Akihutubia kikao hicho, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya aliashiria kipaumbele na umuhimu ilionao kadhia ya Palestina kwa Umoja wa Ulaya na kueleza kwamba, kuna ulazima wa kutayarishwa ajenda maalumu ya utekelezaji kwa ajili ya kuhitimisha mapigano duniani na katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Umoja wa Ulaya, Cairo

Matukio ya kimataifa yanaonyesha kuwa mgororo wa Palestia na haki za wananchi madhulumu wa taifa hilo vinapewa umuhimu mkubwa zaidi duniani. Na hii inadhihirisha kushindwa utawala wa Kizayuni wa Israel na muungaji mkono wake mkuu yaani Marekani, ambazo zimetumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kulitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati kwenye fitna za ugaidi na ukufurishaji ili kuziweka mbali fikra za walimwengu na kadhia ya Palestina.

Hata hivyo vikao mbalimbali vya kimataifa na vya kieneo vinavyofanyika kwa madhumuni ya kuwaunga mkono watu wa Palestina vinathibitisha ukweli huu, kwamba ulimwengu unazidi kulipa umuhimu suala la haki za Wapalestina na kuzidi kulalamikia ughasibu wa utawala wa Kizayuni wa ardhi za Palestina na jinai unazofanya dhidi ya wananchi wa ardhi hiyo.

Mwenendo wa utawala wa Kizayuni umeonyesha kuwa utawala huo ghasibu hauna kiwango wala mpaka katika kutenda jinai zake. Hatua za utawala haramu wa Israel za kupuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa na kukiuka mara kwa mara hati za mikataba ya kimataifa vimezidi kuweka wazi mbele ya walimwengu sura na utambulisho halisi wa utawala huo khabithi.

Mkuu wa Sera za Nje wa EU (wa pili kushoto mstari wa mbele) na Katibu Mkuu wa Arab League (wa tatu kushoto)

Matukio ya kimataifa katika miaka ya karibuni yameonyesha kuwa hatua za kilaghai na kighilba za utawala wa Kizayuni za kupindua ukweli na hakika ya mambo zimepoteza soko na hazikubaliki tena hata mbele ya serikali za nchi za Ulaya ambazo zinahesabika kuwa waungaji mkono wa utawala huo haramu. Kiasi kwamba nchi za Ulaya, ambazo hadi kitambo kidogo tu nyuma zilikuwa zikitambulika kama watetezi na waungaji mkono wa Israel zimeamua kuangalia upya sera zao hizo, kufika hadi sasa kusimama hadharani kuukosoa utawala huo bandia, suala linaloashiria mageuzi katika msimamo wa Ulaya, ambayo hapo kabla ilikuwa daima ikiuetetea na kuuhami kibubusa utawala dhalimu wa Kizayuni.

Mauaji ni moja ya jinai kuu za Israel dhidi ya Wapalestina

Hii ni katika hali ambayo kuongezeka lawama na ukosoaji wa nchi tofauti duniani zikiwemo za mataifa ya Waislamu pamoja na nchi za Ulaya katika miezi ya hivi karibuni dhidi ya hatua za ukandamizaji na za kujipanua za Israel na kuzidi idadi ya nchi zinazopiga kura kwa manufaa ya wananchi wa Palestina katika vikao vya Umoja wa Mataifa kuhusiana na haki za taifa hilo, yote hayo yanaashiria kuzidi kupata nguvu harakati ya uungaji mkono wa pande zote kwa haki za wananchi madhulumu wa Palestina.

Wimbi la kulaani sera za kujipanua na za ukandamizaji za utawala wa Kizayuni katika duru za kimataifa ambalo limesababisha kutengwa zaidi utawala huo haramu kimataifa ni miongoni mwa matunda ya kisiasa na kidiplomasia ya wimbi hilo la kuipinga Israel. Ukweli ni kwamba katika hali ambayo utawala ghasibu wa Israel unajikuta unazidi kubanwa kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kiutamaduni katika uga wa kimataifa kwa jinai unazotenda na kutokana na sera zake za kujipanua, jamii ya kimataifa inaendeleza harakati yake ya kutetea na kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina…/