Mashambulio ya anga ya Saudia yaua raia tisa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22075-mashambulio_ya_anga_ya_saudia_yaua_raia_tisa_yemen
Raia kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulio ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia kusini magharibi mwa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2016 00:20 UTC
  • Mashambulio ya anga ya Saudia yaua raia tisa Yemen

Raia kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulio ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia kusini magharibi mwa Yemen.

Ndege za kivita za Saudia, jana zilishambulia majengo ya makaazi ya raia katika eneo la Far-ul Adin mkoani Ibb. Raia tisa wakiwemo wanawake saba na watoto wawili waliuawa na wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Ndege za utawala vamizi wa Aal Saud zilishambulia pia mara kadhaa kwa makombora eneo la tisa la mji mkuu wa Yemen Sana'a.

Wapiganaji wa kujitolea wa Yemen

Wakati huohuo operesheni ya kulipiza kisasi ya jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea vya wananchi imewaangamiza askari watatu wa Saudia kusini magharibi mwa nchi hiyo. Askari wawili wa Saudia waliuawa katika kituo cha kijeshi cha al-Makhrazaq na mwingine aliuawa katika kituo cha bonde jekundu la mkoa wa Jizan. Aidha magari mawili ya kijeshi ya Saudia yameteketezwa katika shambulio la makombora lililofanywa na vikosi vya jeshi la Yemen.

Vikosi vya jeshi la Yemen vimefanikiwa pia kuteketeza gari la kijeshi na ghala la silaha katika shambulio la makombora dhidi ya kambi ya kijeshi ya al-Misyal iliyoko kwenye eneo la Usair kusini mwa Saudia.

Mwezi Machi mwaka 2015, Saudi Arabia ilianzisha mashambulio dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen. Moja kati ya malengo makuu ya mashambulio hayo ya kivamizi ya utawala wa Aal Saud ni kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake, rais aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abdrabbuh Mansur Hadi.

Abdrabbuh Mansur Hadi

Zaidi ya Wayemeni 11,400 wameshauawa hadi sasa, wengi wao wakiwa ni raia kutokana na mashambulio hayo.../