Israel yafedheheka kwa kutunguliwa ndege yake ya vita huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26598-israel_yafedheheka_kwa_kutunguliwa_ndege_yake_ya_vita_huko_syria
Kufuatia hatua ya hivi karibuni ya kikosi cha Jeshi la Anga la Syria kutungua ndege ya kivita ya utawala haramu wa Israel baada ya ndege hiyo kuingia anga ya Syria, Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa Israel ametishia kushambulia vituo vya silaha za kutungulia ndege vya Syria.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Mar 19, 2017 23:30 UTC
  • Israel yafedheheka kwa kutunguliwa ndege yake ya vita huko Syria

Kufuatia hatua ya hivi karibuni ya kikosi cha Jeshi la Anga la Syria kutungua ndege ya kivita ya utawala haramu wa Israel baada ya ndege hiyo kuingia anga ya Syria, Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa Israel ametishia kushambulia vituo vya silaha za kutungulia ndege vya Syria.

Itakumbukuwa kuwa asubuhi ya Ijumaa iliyopita ndege nne za kivita za utawala katili wa Israel zilikiuka mamlaka ya kujitawala na anga ya Syria kutokea upande wa Lebanon katika eneo la Bureij na kushambulia kambi moja ya jeshi la nchi hiyo wakati ndege hizo zilipokuwa zikielekea mji wa Palmyra, magharibi mwa mji wa Homs.

Ndege ya Israel iliyotunguliwa na jeshi la Syria

Wakati huo jeshi la Syria lilikabiliana na hujuma hiyo na kutungua mojawapo ya ndege hizo, huku zingine zikilazimika kukimbia baada ya kuzidiwa. Kufuatia radiamali hiyo ya jeshi la Syria iliowatia wasiwasi mkubwa watawala wa Kizayuni, Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa Israel ameibuka na kudai kuwa, katika mashambulizi ya baadaye, jeshi la anga la utawala huo litayalenga maeneo ya Jeshi la Anga la Syria na kuyasambaratisha.

Ndege ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel

Baada ya tukio la siku ya Ijumaa, Komandi la ya Jeshi la Anga nchini Syria iliionya Israel kwamba ikiwa chokochoko za namna hiyo zitakaririwa, jeshi hilo litatumia nguvu kutoa jibu kali.

Tangu mgogoro wa Syria ulipoibuka hapo mwezi Machi mwaka 2011, utawala haramu wa Israel kwa mara kadhaa umekuwa ukituma misaada mbalimbali kwa makundi ya kigaidi hususan Daesh, Jab'hatu Nusra na mfano wa hayo huko Syria, huku jeshi lake likishambulia maeneo ya jeshi la Syria.