Ombi la UN kwa Iran, Russia, na Uturuki kuhusu Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26878-ombi_la_un_kwa_iran_russia_na_uturuki_kuhusu_syria
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria kwa mara nyingine tena amezitaka Iran, Russia na Uturuki kufanya juhudi za kulinda usitishaji vita huko Syria.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Mar 26, 2017 03:43 UTC
  • Ombi la UN kwa Iran, Russia, na Uturuki kuhusu Syria

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria kwa mara nyingine tena amezitaka Iran, Russia na Uturuki kufanya juhudi za kulinda usitishaji vita huko Syria.

Stephen de Mistura amewatumia barua Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Uturuki na Iran akiwataka kuchukua hatua haraka ili kulinda usitishaji vita huko Syria na kuandaa njia ya mazungumzo ya amani. Katika barua hiyo, De Mistura imezitolea wito Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na Uturuki kulinda usitishaji vita huko Syria ili kuboresha hali ya mambo na kuandaa mazingira ya kusonga mbele mchakato wa kisiasa nchini Syria.

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria juzi Ijumaa aliunga mkono juhudi za Russia, Uturuki na Iran kuhusu Syria na kutaka kuendelezwa mchakato huo ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Stephen de Mistura na ujumbe wa serikali ya Syria mkutanoni Geneva, Uswisi 

Mgogoro ulianza nchini Syria mwaka 2011 kufuatia hujuma na mashambulizi makubwa ya makundi ya kigaidi yakiungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wake kwa lengo la kuing'oa madarakani serikali halali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Bashar al Assad.