Waarabu wajidhalilisha kwa kutaka kufanya 'mapatano ya kihistoria' na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27036-waarabu_wajidhalilisha_kwa_kutaka_kufanya_'mapatano_ya_kihistoria'_na_israel
Viongozi wa nchi za Kiarabu wamemaliza kikao chao cha siku moja cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kilichofanyika nchini Jordan kwa kutangaza kuwa wako tayari kufanya kile walichokiita 'mapatano ya kihistoria' na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 29, 2017 22:46 UTC
  • Waarabu wajidhalilisha kwa kutaka kufanya 'mapatano ya kihistoria' na Israel

Viongozi wa nchi za Kiarabu wamemaliza kikao chao cha siku moja cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kilichofanyika nchini Jordan kwa kutangaza kuwa wako tayari kufanya kile walichokiita 'mapatano ya kihistoria' na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa iliyosomwa mwishoni mwa kikao hicho na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Ahmad Abul-Ghaith, imeeleza kuwa Waarabu wako tayari kufanya mapatano hayo kwa sharti kwamba Israel iondoke kwenye ardhi ilizozivamia na kuanza kuzikalia kwa mabavu katika vita vya mwaka 1967.

Viongozi wa Waarabu waliokutana Jordan

Kutangaza rasmi Arab League mpango wa Waarabu wa kufanya mapatano na utawala haramu wa Israel kunajiri katika hali ambayo katika miaka ya karibuni watawala wa nchi nyingi za Kiarabu na hasa wa Saudi Arabia na Bahrain wameanzisha kimya kimya na kwa njia isiyo rasmi uhusiano na utawala unaoikalia kwa mabavu Quds, kilipo kibla cha kwanza cha Waislamu, na ambao ni adui mkuu wa wananchi wa Palestina na Ulimwengu wa Kiislamu. 

Quds tukufu, ulipo msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Alam, taarifa ya mwisho ya kikao cha Jordan imesisitiza juu ya kuendelezwa mazungumzo ya mapatano baina ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel kwa msingi wa njia ya utatuzi ya kuundwa nchi mbili pasina kuzingatia matakwa ya wananchi wa Palestina.

Wananchi pamoja na makundi ya wanamapambano wa Palestina daima wamekuwa wakiitakidi kuwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel ni hatari kubwa kwa Wapalestina na kwamba kuendelezwa mazungumzo ya mapatano, kila mara kumekuwa na madhara kwa Wapalestina.../