Umoja wa Mataifa wapinga tena ujenzi wa vitongoji vya walowezi, Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27120-umoja_wa_mataifa_wapinga_tena_ujenzi_wa_vitongoji_vya_walowezi_palestina
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema taasisi hiyo ya kimataifa ina wasiwasi juu ya kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 31, 2017 23:37 UTC
  • Umoja wa Mataifa wapinga tena ujenzi wa vitongoji vya walowezi, Palestina

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema taasisi hiyo ya kimataifa ina wasiwasi juu ya kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Stéphane Dujarric amesema kuwa, umoja huo unapinga hatua hiyo ya upande mmoja inayohatarisha amani ya kimataifa na kudhoofisha uundaji wa taifa huru la Palestina. 

Wakati huo huo mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina, Hanana Ashrawi amesema Israel inaendeleza ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina, suala ambalo ni ukiukaji wa wazi wa sheria na maazimio ya kimataifa. 

Vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, Palestina

Alkhamisi iliyopita utawala haramu wa Israel ulidharau tena maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi huko Palestina. 

Maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yalailazimisha Israel kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina na kubomoa vitongoji vyote vilivyojengwa katika katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.