90% ya mji wa Mosul wakombolewa, Magaidi 170 wauawa Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29176-90_ya_mji_wa_mosul_wakombolewa_magaidi_170_wauawa_iraq
Kamanda wa Operesheni ya Jeshi la Iraq ametangaza habari ya kukombolewa asilimia 90 ya maeneo ya magharibi mwa mji wa Mosul yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 16, 2017 09:56 UTC
  • 90% ya mji wa Mosul wakombolewa, Magaidi 170 wauawa Iraq

Kamanda wa Operesheni ya Jeshi la Iraq ametangaza habari ya kukombolewa asilimia 90 ya maeneo ya magharibi mwa mji wa Mosul yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Msemaji wa Operesheni ya Jeshi la Iraq, Brigedia Jenerali Yahya Rasool amewaambia waandishi wa habari leo Jumanne mjini Baghdad kuwa, kwa sasa magaidi wa takfiri wa Daesh wanadhibiti asilimi 10 tu ya eneo hilo, mashariki mwa fuo za Mto Tigris baada ya kupata pigo la kijeshi.

Amesema katika kipindi cha siku chache zijazo, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu bendera ya Iraq itapepea magharibi mwa mji wa Mosul na kwamba watakuwa wameuteka kikamilifu mji huo.

Wanajeshi wa Iraq, magharibi mwa Iraq

Hii ni katika hali ambayo, magaidi 173 wa kundi la ukufurishaji la Daesh (ISIS) waliangamizwa jana Jumatatu katika operesheni ya kulikomboa eneo la magharibi mwa mji wa Mosul, iliyofanywa na jeshi la Iraq likishirikiana na wapiganaji wa kujitolea. 

Magaidi zaidi ya 16,400 wa Daesh wameuawa tangu operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul kutoka katika makucha ya magaidi wa Daesh katika mkoa wa Nainawa ilipoanza mwezi Oktoba mwaka jana kwa amri ya Haidar al Abadi, Waziri Mkuu wa Iraq ambapo vikosi vya Iraq vimefanikiwa kulikomboa eneo la mashariki mwa Mosul na hivi sasa wanakaribia kulikomboa eneo la magharibi mwa mji huo.