UN yaitaka Israel iache kuyakalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29346-un_yaitaka_israel_iache_kuyakalia_kwa_mabavu_maeneo_ya_wapalestina
Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukome kuzikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 20, 2017 08:15 UTC
  • UN yaitaka Israel iache kuyakalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina

Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukome kuzikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.

Michael Lynk, ripota wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesisitizia wajibu wa  Israel kuacha kuzikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na kusema kuwa, hali ya kibinadamu huko Palestina ni ya kutia wasiwasi mkubwa.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa matamshi hayo baada ya ziara yake ya siku tano katika eneo hilo na amelaani hatua ya Israel ya kuendelea na vitendo vyake vyenye shabaha maalumu vya uvunjaji wa haki za Wapaelstina ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu ya kiumati dhidi ya Wapelestina, kuwapora mali zao, kutumia nguvu dhidi yao, kuwaua bila sababu, kuwapiga marufuku kutoka nje, kutowapa uhuru wa kwenda wanakotaka, kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuwalazimisha Wapalestina kuyahama kwa nguvu maeneo yao.

Mwanamke Mpalestina akiwa amesimama imara mbele ya wanajeshi wa Israel kulalamikia kuporwa ardhi zao

 

Ripota huyo wa Umoja wa Mataifa amesema hayo baada ya kufanya ziara ya siku tano katika eneo hilo na kuitaka jamii ya kimtaifa iongeze juhudi za kukomesha kukaliwa kwa mabavu na Israel maeneo ya Wapalestina, kukomeshwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kupata Wapalestina haki yao ya kujiamulia wenyewe mustakbali wao. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel ni maarufu kwa kukaidi sheria za kimataifa, kuvunja haki za binadamu na ni maarufu pia kwa kukosa uaminifu na kukanyaga hata makubaliano unayoyatia saini kwa hiari yake.