Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia tena Msikiti wa al -Aqswa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29760-makumi_ya_walowezi_wa_kizayuni_wavamia_tena_msikiti_wa_al_aqswa
Makumi ya walowezi wa Kizayuni leo wamevamia tena Msikiti wa al Aqsa kupitia upande wa Bab al-Magharibah na kwa mara nyingine tena kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2017 09:43 UTC
  • Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia tena Msikiti wa al -Aqswa

Makumi ya walowezi wa Kizayuni leo wamevamia tena Msikiti wa al Aqsa kupitia upande wa Bab al-Magharibah na kwa mara nyingine tena kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.

Ripoti zinasema kuwa, polisi ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliandaa mazingira ya kiusalama kwa ajili ya kuingia katika eneo hilo walowezi hao wa Kizayuni, eneo tukufu ambalo ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Sambamba na uvamizi huo wa walowezi wa Kizayuni, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel leo wamevamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia mbaroni Wapalestina wapatao 12.

Wapalestina waliotiwa mbaroni ni wenyeji wa Quds, Ramallah, Beit Lahm, Nablos, Qalqiliya na al-Khalil. Uvamizi huo wa leo wa jeshi la Israel umezusha wasiwasi mkubwa wananchi wa maeneo hayo ambao wako katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wapalestina hutiwa mbaroni kila siku na wanajeshi wa Israel

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya juhudi za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina. Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama zake za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Baytul Muqaddas. 

Hadi sasa Wapalestina zaidi ya 200 wameshauawa shahidi na utawala haramu na wa Kizayuni wa Israel tangu lilipozuka wimbi la Intifadha ya Quds Oktoba mwaka juzi, huku wengine wengi wakiendelea kuitiwa mbaroni.