UN yataka kukomeshwa mapigano Masjidul Aqsa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31966-un_yataka_kukomeshwa_mapigano_masjidul_aqsa
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa mapigano yanayoendelea katika Msikiti mtakatifu wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 19, 2017 07:15 UTC
  • UN yataka kukomeshwa mapigano Masjidul Aqsa

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa mapigano yanayoendelea katika Msikiti mtakatifu wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq ameashiria ukatili unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji wa Quds na kutoa wito wa kukomeshwa machafuko na mapigano katika Msikiti wa al Aqsa. 

Kuhusu hatua mpya zilizochukuliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Baitul Muqaddas na Msikiti wa al Aqsa, Farhan Haq amesema kuwa, hali ya mji wa Baitul Muqaddas inapaswa kubakia kama ilivyokuwa. 

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametoa wito wa kuitishwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kwa shabaha ya kujadili njia za kukabiliana na hatua mpya za utawala haramu wa Israel katika mji wa Baitul Muqaddas na Msikiti wa al Aqsa.

Msikiti wa al Aqsa

Rami Hamdallah amezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kutekeleza majukumu yao ya kuilinda Quds na matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika mji huo. 

Ijumaa iliyopita utawala wa Kizayuni wa Israel ulifunga milango yote ya kuingia katika Msikiti wa al Aqsa na kuwazuia Waislamu kutekeleza ibada ya Swala ndani ya msikiti huo baada ya mapigano yaliyotokea baina ya raia wa Palestina na askari wa utawala huo. Wapalestina 3 waliuawa shahidi katika mapigano hayo na askari wawili wa Israel waliangamizwa.