Mar 17, 2016 09:24 UTC
  • Ban alaani jinai mpya za Saudia nchini Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani jinai mpya zilizofanywa na utawala wa Saudi Arabia baada ya kushambulia soko la Khamis katika mkoa wa Hajjah huku kaskazini magharibi mwa Yemen.

Ban Ki-moon amelaani vikali jinai na mauaji yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia baada ya kushambulia soko lililokuwa limefurika watu la Khamis na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji hayo ya kutisha.

Katika upande mwingine Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka pia imelaani mashambulizi hayo ya anga ya Saudi Arabia yaliyolenga soko na kusema kuwa, timu ya madaktari wa jumuiya hiyo inashughulikia makumi ya majeruhiwa wa mashambulizi hayo katika hospitali ya Abas kwenye mkoa wa Hajjah.

Awali harakati ya Ansarullah ilikuwa imetoa taarifa ikilaani vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudia dhidi ya soko la Khamis.

Jumanne iliyopita ndege za kivita za Saudia zilishambulia soko la Khamis na kuua raia 107. Watu wengine 90 walijeruhiwa.

Tags