Iran na Russia kuendelea kushirikiana kuhusu mgogoro wa Syria
Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Iran na Russia wamesisitizia udharura wa kuendelezwa mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria, sambamba na kupambana na magenge ya kigaidi.
Katika mkutano mjini Moscow jana Jumanne, Hossein Jaberi Ansari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Ujumbe wa Russia eneo la Mashariki ya Kati Mikhail Bogdanov wamesema kuna haja mazungumzo ya Astana nchini Kazakhstan kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mzozo wa Syria yaendelee.
Kadhalika maafisa hao wa Iran na Russia wamesema kuna umuhimu wa kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa raia wa Syria, kuwarejesha wakimbizi katika makazi yao na kuunda ramani ya njia ya kuzingatiwa baada ya mgogoro huo.
Katika hali ambayo Iran na Russia zimekuwa zimekifanya jitihada za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo, Marekani kwa upande wake imekuwa ikitoa madai ya uongo kwamba Syria inatumia silaha za kemikali dhidi ya raia na hivyo kuleta anga ya vita vya kisaikolojia dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu na wakati huo huo kuyaandalia mazingira makundi ya kigaidi ya kutekeleza vitendo vya kigaidi.
Mbali na Israel na Marekani, nchi za Kiarabu nazo zimeendelea kuyaunga mkono makundi ya kigaidi yanayoipiga vita serikali halali ya Rais Bashar al-Assad.
Tehran na Moscow zimekuwa zikisisitiza kuwa, mapambano halisi na ya kweli dhidi ya ugaidi na kurejesha amani ya kudumu katika eneo la Mashaiki ya Kati ni lengo la pamoja la Iran na Syria.