Kuwait yakadhibisha madai ya Reuters dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32616
Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait imetoa taarifa ikikadhibisha madai ya shirika la habari la Reuters kwamba Iran inatumia maji ya Kuwait kutuma silaha kwa harakati ya Ansarullah ya Yemen.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 03, 2017 02:33 UTC
  • Kuwait yakadhibisha madai ya Reuters dhidi ya Iran

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait imetoa taarifa ikikadhibisha madai ya shirika la habari la Reuters kwamba Iran inatumia maji ya Kuwait kutuma silaha kwa harakati ya Ansarullah ya Yemen.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait jana Jumatano ilitangaza katika taarifa yake kuwa maji ya kieneo ya nchi hiyo yanadhibitiwa kwa nyenzo zote na yako chini ya uangalizi kamili wa kikosi cha baharini na cha pwani ya nchi hiyo usiku na mchana. Kuwait imesema kuwa hadi sasa haijashuhudia harakati zozote zinazotia shaka katika maeneo ya baharini yaliyo chini ya udhibiti wake.

Wapiganaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen  

Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imeviomba vyombo vya habari vya kieneo kutotangaza habari zozote zisizo sahihi na za uwongo. Mwezi Machi uliopita shirika la habari la Reuters lilivinukuu vyombo vya nchi za Kiarabu na kudai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetumia maji yaliyo baina ya Kuwait na Iran kwa ajili ya kutuma silaha kwa harakati ya Ansarullah ya huko Yemen.