Wanajeshi na mamluki wa Saudi Arabia waendelea kuangamizwa nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i343-wanajeshi_na_mamluki_wa_saudi_arabia_waendelea_kuangamizwa_nchini_yemen
Wanajeshi zaidi ya 200 wa Saudia wameuawa na magari na zana za kijeshi za nchi hiyo kuharibiwa vibaya katika shambulio lililofanywa na jeshi la Yemen katika kituo cha anga cha al Anad kusini mwa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2016 23:25 UTC
  • Wanajeshi na mamluki wa Saudi Arabia waendelea kuangamizwa nchini Yemen

Wanajeshi zaidi ya 200 wa Saudia wameuawa na magari na zana za kijeshi za nchi hiyo kuharibiwa vibaya katika shambulio lililofanywa na jeshi la Yemen katika kituo cha anga cha al Anad kusini mwa Yemen.

Habari zinasema kuwa, mamluki wengi wa Saudia waliokuweko kwenye kambi hiyo walikuwa ni wanajeshi wa Sudan.

Kwa mara ya kwanza jeshi la Sudan limethibitisha kuuliwa mwanajeshi wake mmoja huko Yemen. Ahmad Khalifa al Shami msemaji wa jeshi la Sudan ndiye aliyetangaza habari hiyo. Sudan ilijiunga na muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Saudi Arabia ilianzisha vita dhidi ya wananchi wa Yemen tangu mwezi Machi mwaka jana, na imekuwa ikishambulia kwa ndege za kivita maeneo mbalimbali ya raia wa Yemen, na kuuwa maelfu ya watu wasio na hatia kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakani Rais aliyetoka nchi wa Yemen.

Shambulio la jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya raia wa nchi hiyo katika kambi ya kijeshi ya al Anad limesababisha pia kuuliwa Nicolaus Petros kamanda wa Kimarekani aliyekuwa akiongoza kikosi chenye uhusiano na shirika la Black Water katika kambi ya al Anad kusini mwa Yemen.