Sheikh Maher Hamoud: Muda wa kusambaratishwa Israel umekaribia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i38311-sheikh_maher_hamoud_muda_wa_kusambaratishwa_israel_umekaribia
Sheikh Maher Hamoud, Mkuu wa Umoja wa Ulimwengu wa Maulama wa Muqawama wa nchini Lebanon amesema kuwa, muda wa kusambaratishwa utawala haramu wa Kizayuni umekaribia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 30, 2017 11:32 UTC
  • Sheikh Maher Hamoud: Muda wa kusambaratishwa Israel umekaribia

Sheikh Maher Hamoud, Mkuu wa Umoja wa Ulimwengu wa Maulama wa Muqawama wa nchini Lebanon amesema kuwa, muda wa kusambaratishwa utawala haramu wa Kizayuni umekaribia.

Sheikh Hamoud sambamba na kusisitizia ulazima wa kusambaratika utawala wa Israel amesema kwamba, haujabakia muda mwingi kabla ya kusambaratishwa utawala huo. Hata hivyo ameongeza kwamba hiyo haina maana ya kukaa na kusubiria hatma ya kusambaratika adui huyo Mzayuni. Amesema mataifa ya Kiarabu na Waislamu wote ni lazima washiriki katika kuhitimisha uvamizi wa utawala huo haramu huko Palestina. 

Sheikh Maher Hamoud, Mkuu wa Umoja wa Ulimwengu wa Maulama wa Muqawama

Mkuu wa Umoja wa Ulimwengu wa Maulama wa Muqawama sambamba na kukosoa vikali njama za baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu wanaotaka kuboresha mahusiano na utawala wa Kizayuni amesema kuwa, wale wanaoshirikiana na adui sambamba na kuufanyia uadui muqawama, lazima watakumbwa na hatma ya kufedhehesha. Sheikh Maher Hamoud ambaye ni alimu wa Kisuni nchini Lebanon anatambulika kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono muqawama unaopambana na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu na Warabu.