Syria yatungua ndege ya kivita ya Israel aina ya F-16
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40193-syria_yatungua_ndege_ya_kivita_ya_israel_aina_ya_f_16
Jeshi la Syria limetungua ndege moja ya kivita ya utawala haramu wa Israeli aina ya F-16 ambayo ilikuwa imetekekeza hujuma ndani ya ardhi ya Syria mapema leo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 10, 2018 13:11 UTC
  • Syria yatungua ndege ya kivita ya Israel aina ya F-16

Jeshi la Syria limetungua ndege moja ya kivita ya utawala haramu wa Israeli aina ya F-16 ambayo ilikuwa imetekekeza hujuma ndani ya ardhi ya Syria mapema leo.

Televisheni ya taifa ya Syria imemnukuu afisa wa kijeshi akisema kituo cha ulinzi wa anga kimetoa jibu kali kwa uvamizi wa Israel dhidi ya kituo cha ndege za kijeshi kati mwa Syria. Afisa hiyo aidha amedokeza kuwa, ni zaidi ya ndege moja ilivyotunguliwa.

Jeshi la utawala haramu wa Israel limethibitisha kuwa, ndege yake ya kivita aina ya F-16 imedondoshwa kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel na kuongeza kuwa, marubani waliweza kuruka kwa mwavuli kutoka ndani ya ndege hiyo kabla  haijaanguka na kuteketea kikamilifu. Taarifa zinasema hali ya rubani huyo wa Kizayuni ni mahututi.

Ndege iliyotunguliwa ikiteketea

Wakati huo huo Fawzi Barhoum Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amepongeza hatua ya Syria kutungua ndege hiyo ya Israel na kusema ni jibu tarajiwa kwa hujuma ya utawala huo.