Wazayuni wazidi kuua Wapalestina baada ya kukingiwa kifua na Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i42692-wazayuni_wazidi_kuua_wapalestina_baada_ya_kukingiwa_kifua_na_saudia
Utawala wa Kizayuni wa Israel umezidisha mashambulizi na mauaji dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina hasa baada ya Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia kutangaza hadharani kuwa Wazayuni wana haki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2018 10:22 UTC
  • Wazayuni wazidi kuua Wapalestina baada ya kukingiwa kifua na Saudia

Utawala wa Kizayuni wa Israel umezidisha mashambulizi na mauaji dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina hasa baada ya Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia kutangaza hadharani kuwa Wazayuni wana haki.

Habari za hivi karibuni zinasema kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kinyama waliyofanyiwa na wanajeshi katili wa Israel katika maandamano ya amani ya Wapalestina hao ya siku ya Ijumaa imefikia watu 20.

Shirika la habari la Mehr limesema kuwa, Shadi Hamdan, kijana wa Kipalestina aliyejeruhiwa vibaya katika maandamano ya amani ya siku ya Ijumaa ya tarehe 30 Machi ya kupigania kurejea makwao wakimbizi wa Palesitna amekufa shahidi leo kutokana na majeraha.

Israel imetumia silaha za kivita kuwashambulia Wapalestina waliokuwa wanaandamana kwa amani kupigania haki zao. Saudia yasema Wazayuni wana haki na Riyadh inapigania kuimarisha uhusiano wake na Israel

 

Hadi hivi sasa zaidi wa Wapalestina 1,900 wameshajeruhiwa tangu Ijumaa iliyopita kutokana na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa upande wake televisheni ya al Alam imetangaza leo kuwa, Mpalestina mmoja ameuawa shahidi baada ya ndege isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi mashariki mwa mji wa Ghaza.

Makundi mbalimbali ya Palestina yanaendelea kulaani matamshi ya Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ambaye hivi karibuni aliliambia Jarida la Atlantic la Marekani, kwamba Saudia na utawala haramu wa Israel zina maslahi ya pamoja na iwapo zitakuwa na uhusiano wa wazi, basi utawala huo pandikizi utapata faida kubwa na pia nchi za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi nazo zitafaidika.

Hivi karibuni pia Saudi Arabia iliruhusu anga yake itumiwe na ndege zinazoelekea Israel, hatua ambayo inaonesha kuzidi kuimarika uhusiano wa ukoo wa Aal Saud na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao una faili jeusi mno la jinai dhidi ya wananchi wa Palestina.