Wizara ya Afya ya Palestina: Hospitali zote za Gaza zinakaribia kufungwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46997-wizara_ya_afya_ya_palestina_hospitali_zote_za_gaza_zinakaribia_kufungwa
Wizara ya Afya ya Palestina imetahadharisha kuwa hospitali na vituo vyote vya afya katika eneo la Ukanda wa Gaza vinakaribia kufungwa kutokana na kuishiwa na nishati ya kuendeshea mitambo ya umeme.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 24, 2018 20:49 UTC
  • Wizara ya Afya ya Palestina: Hospitali zote za Gaza zinakaribia kufungwa

Wizara ya Afya ya Palestina imetahadharisha kuwa hospitali na vituo vyote vya afya katika eneo la Ukanda wa Gaza vinakaribia kufungwa kutokana na kuishiwa na nishati ya kuendeshea mitambo ya umeme.

Mkurugenzi wa Idarara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Wizara ya Afya ya Palestina, Ashraf Abu Mahadi amesema kuwa nishati iliyotumwa na baadhi ya nchi za Kiislamu huko Gaza itamalizika wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi ujao na hii ina maana ya kufungwa kabisa vituo vyote vya huduma za afya na kushadidi mgogoro wa wakazi wa Gaza.

Ashraf Abu Mahadi ameongeza kuwa, baada ya umeme wa Ukanda wa Gaza kukatwa kwa masaa 16 kwa siku, mitambo ya kuzalisha umeme ya eneo hilo ndiyo inayofidia nakisi hiyo lakini jenereta hizo pia zinahitaji utunzani na nishati.

Ukanda wa Gaza unazingirwa na Wazayuni kwa miaka mingi

Abu Mahadi amezitaka taasisi za kimataifa, nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za dharura za kudhamini nishati ya kutosha kwa ajili ya jenereta za hospitali na vituo vya afya katika eneo la Ukanda wa Gaza. 

Eneo hilo la Palestina ambalo lina wakazi karibu milioni mbili limekuwa chini ya mzingoro mkali wa baharini, angani na nchi kavu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa miaka mingi sasa na linasumbuliwa na uhaba mkubwa na nishati, dawa, chakula na huduma nyingine muhimu.