Saudia yawapiga marufuku mahujaji kujadili masuala ya Yemen na Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47077-saudia_yawapiga_marufuku_mahujaji_kujadili_masuala_ya_yemen_na_palestina
Kufuatia kushindwa siasa za Saudia kuanzia nchini Syria, Iraq na Yemen, na kadhalika kashfa za kuyasaidia kifedha makundi ya kigaidi na Kiwahabi, serikali ya Riyadh imepiga marufuku vikao vya aina yoyote vinavyojadili masuala ya kisiasa yakiwemo masuala ya Yemen na Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2018 06:52 UTC
  • Saudia yawapiga marufuku mahujaji kujadili masuala ya Yemen na Palestina

Kufuatia kushindwa siasa za Saudia kuanzia nchini Syria, Iraq na Yemen, na kadhalika kashfa za kuyasaidia kifedha makundi ya kigaidi na Kiwahabi, serikali ya Riyadh imepiga marufuku vikao vya aina yoyote vinavyojadili masuala ya kisiasa yakiwemo masuala ya Yemen na Palestina.

Katika kuendeleza mashinikizo ya Saudia dhidi ya nchi za Waislamu kwa kutumia ibada ya Hija, wajumbe wa Baraza la Masuala ya Kisalama na Kisiasa nchini Saudia sambamba na kufanya kikao kilichoongozwa na Mohammad bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo kwa ajili ya kujadili masuala ya eneo la Mashariki ya Kati na kimataifa, wamepiga marufuku vikao vyote vya masuala ya kisiasa vinavyojadili masuala ya Yemen na Palestina.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa masuala ya kisheria, hivi sasa Saudia inaendesha ibada ya Hija katika fremu ya kutekeleza ajenda maalumu za kisaisa, jambo ambalo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Al-Kaabah, ambayo inashuhudia usiasa wa utawala wa Aal-Saud

Tarehe 17 mwezi huu pia Kamati ya Kimataifa ya Usimamizi wa Haramu Mbili (Makkah na Madina) pia iliziandikia barua tofauti Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Kamisheni ya Masuala ya Kidini na Uhuru wa Kujieleza ya Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Bunge la Umoja wa Ulaya, ikiishtaki Saudia kutokana na kuingiza masuala ya kisiasa katika ibada ya Hija na kuminya uhuru wa kujieleza na wa kidini.

Katika kutekeleza mashinikizo dhidi ya nchi zinazopinga siasa za utawala wa Aal-Saud, serikali ya Riyadh pia imewazuia raia wengi wa nchi za Kiislamu ikiwemo Yemen, Syria na Qatar kwenda kutekeleza ibada ya Hija nchini humo.