UN Yasikitishwa na Hujuma ya Saudia dhidi ya Hospitali Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47220-un_yasikitishwa_na_hujuma_ya_saudia_dhidi_ya_hospitali_yemen
Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amebainisha masikitiko yake kufuatia hatua ya muungano unaoongozwa na Saudia kushambulia hospitali na soko katika mji wa Al Hudaydah nchini Yemen.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Aug 04, 2018 03:42 UTC
  • UN Yasikitishwa na Hujuma ya Saudia dhidi ya Hospitali Yemen

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amebainisha masikitiko yake kufuatia hatua ya muungano unaoongozwa na Saudia kushambulia hospitali na soko katika mji wa Al Hudaydah nchini Yemen.

Siku ya Alhamisi ndege za kivita za muungano unaoongozwa na Saudia ulitumia ndege za kivita kudondosha mabomu katika  hospitali na soko katika Bandari ya Al Hudaydah ambapo raia zaidi ya 60 waliuawa na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa. Kati ya raia wasio na hatia waliopoteza maisha katika jinai hiyo mpya ya kivita ya Saudi Arabia ni wanawake na watoto wachanga.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu Yemen Lise Grand amesema hali hiyo ni ya “kushangaza na kusikitisha, hospital zinalindwa chini ya sheria za kimataifa za binadamu na hakuna chochote kinachohalalisha upotevu huo wa maisha ya binadamu.”

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis Ijumaa kuhusu shambulio hilo msemaji wa OCHA Jens Laerke amenukuu tarifa ya Lise Granda na kusema: “Al Thawra ndio hospital kubwa nchini Yemen na moja ya hospital chache zinazofanya kazi katika eneo hilo. Ina moja ya vituo bora zaidi vya kutibu kipindupindu mjini humo, mamia kwa maelfu ya watu wanategemea hospitali hiyo ili kuishi." Ameongeza kuwa pande zote kinzani katika mzozo wa Yemen zina wajibu kimataifa kuwalinda raia na miundombinu yao kwa kufanya kila liwezekanalo , na huo sio wajibu wa hiyari bali ni wa lazima.

Watoto ni waathirika wakuu wa jinai za Saudia nchini Yemen

Hivi sasa mgogoro wa Yemen ndio mbaya kuliko yote duniani , watu milioni 22 sawa na asilimia 75 ya watu wote wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio