Uingereza yalaumiwa kwa kuzuia kutangazwa ukweli kuhusu Palestina
Zaidi ya mashirika 80 yanayojishughulisha na masuala haki za watu weusi na watu wenye asili ya Asia pamoja na jamii ya wachache nchini Uingereza yamesema kuwa, kuna njama za makusudi zinafanyika nchini humo kuzuia kujadiliwa na kuwekwa wazi kadhia ya Palestina.
Gazeti la al Quds al Arabi limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mashirika hayo yamesema, inasikitisha kuona kuwa kila mtu anayetangaza ukweli kuhusu Palestina anapachikwa jina la "adui wa Mayahudi" kwa lengo la kuzuia kufanyika uchunguzi wa kina wa kihistoria kuhusiana na Palestina.
Itakumbukwa kuwa, katika hati ya "Muungano wa Kimataifa wa Kumbukumbu za Holocaust" iliyotolewa mwaka 2016 na wafuasi wa utawala wa Kizayuni wa Israel, kulitolewa orodha ya maneno ambayo yanapotumika huwa na maana ya kuwa na uadui na Mayahudi kwa mujibu wa muungano huo.
Kwa mujibu wa hati hiyo, ni marufuku kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi.
Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu ya Uingereza yamelaani hati ya muungano huo ambao lengo lake hasa ni kukuza kupindukia ngano ya Holocaust kwa faida ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Hati hiyo imepiga marufuku pia kufananishwa jinai za utawala wa Kizayuni na siasa za Wanazi wa Ujerumaini kama ambavyo imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu mijadala inayofanyika juu ya matukio ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948.