Wapalestina: Marekani inajaribu kuturubuni kimabavu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47708-wapalestina_marekani_inajaribu_kuturubuni_kimabavu
Mbunge mmoja wa Palestina amesema kuwa, uamuzi wa Marekani wa kukatisha misaada yake kwa Wapalestina ni kujaribu kuwarubuni kimabavu ili wakubaliane na mpango wa "Muamala wa Karne" wa kuiangamiza kikamilifu kadhia ya Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 26, 2018 22:49 UTC
  • Wapalestina: Marekani inajaribu kuturubuni kimabavu

Mbunge mmoja wa Palestina amesema kuwa, uamuzi wa Marekani wa kukatisha misaada yake kwa Wapalestina ni kujaribu kuwarubuni kimabavu ili wakubaliane na mpango wa "Muamala wa Karne" wa kuiangamiza kikamilifu kadhia ya Palestina.

Serikali ya Marekani imesema kuwa imeamua kukatisha misaada ya kifedha ya dola milioni 200 kwa shirika la UNRWA la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina na badala yake itatumia fedha hizo kuendeshea miradi yake mingine.

Bi Hanan Ashrawi amenukuliwa na shirika la habari la IRIB akisema jana (Jumapili) kwamba, serikali ya Donald Trump huko Marekani inajaribu kuwarubuni kimabavu Wapalestina na kwamba kuna kundi fulani katika Ikulu ya nchi hiyo (White House) ambalo kwa hakika ni la Wazayuni wenye misimamo mikali ambao wanaiangalia Palestina kiubaguzi na kiunyanyasaji.

Wakimbizi wa Palestina katika kituo cha shirika la misaada la Umoja wa Mataifa UNRWA

 

Kiongozi huyo mwandamizi wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO aidha amesema, uamuzi huo wa Marekani si wa kiuadilifu hata kidogo. 

Amesema, serikali ya Marekani imethibitisha kuwa ni tabia yake kutumia mabavu kuzilazimisha pande nyingine kufanya inavyotaka lakini wananchi na viongozi wa Palestina kamwe hawatosalimu amri mbele ya vitisho hivyo ya Marekani na wanasema hadharani kuwa, haki za Wapalestina si kitu cha kupigiwa mnada au kufanyiwa udalali wa bei.