Syria mwaka 2018 iliuza bidhaa zake katika nchi 90 duniani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51382-syria_mwaka_2018_iliuza_bidhaa_zake_katika_nchi_90_duniani
Muungano wa Jumuiya za Syria zinazouza bidhaa nje ya nchi umetangaza kuwa, mwaka uliopita wa 2018 nchi hiyo iliuza bidhaa kwa nchi 90 duniani zikiwemo zile ambazo zilikuwa zimeiwekea vikwazo Damascus.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Feb 06, 2019 23:26 UTC
  • Syria mwaka 2018 iliuza bidhaa zake katika nchi 90 duniani

Muungano wa Jumuiya za Syria zinazouza bidhaa nje ya nchi umetangaza kuwa, mwaka uliopita wa 2018 nchi hiyo iliuza bidhaa kwa nchi 90 duniani zikiwemo zile ambazo zilikuwa zimeiwekea vikwazo Damascus.

Muungano huo umeashiria kurejea uzalishaji wa asilimia 80 wa bidhaa za Syria  katika masoko ya kimataifa baada ya mgogoro wa nchi hiyo na kuongeza kuwa: Bidhaa zilizozalishwa Syria katika muda wa miezi tisa zimeuzwa kwa makumi ya nchi jirani na zile za pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi, Ulaya, Marekani, Japan, China na katika aghalabu ya nchi za Asia na bara Amerika.  

Uzalishaji huo unajumuisha mazao ya kilimo na viwanda kama bidhaa za nguo, kazi za mikono, bidhaa za petrokemikali na huduma za uhandisi ambazo zimekuwa na nafasi muhimu katika kufufua uchumi wa Syria baada ya miaka saba ya vita, kuzingirwa na kuwekewa vikwazo nchi hiyo. 

Bidhaa za nguo zinazozalishwa nchini Syria 

Gazeti la Rai al Yaum huko limeshiria safari za viongozi wa nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu mjini Damascus huko Syria  na kuandika kuwa: Baada ya kupita miaka saba ya vita huko nchini humo, nchi hizo sasa zinataka kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Damascus.