Iraq yachunguza kuuzwa kwa wanawake wa Kiizadi katika nchi za Kiarabu
Mwakilishi wa zamani wa kaumu wa Waizadi katika Bunge la Iraq amesema mpango wa kufanyika uchunguzi kuhusu ripoti ya kuuzwa wanawake wa kaumu hiyo huko Saudi Arabia na katika nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi ungali unaendelea.
Hajji Kandour al Sheikh amesema ripoti zinaonesha kuwa, wanawake wa Kiizadi waliotekwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wamepelekwa na kuuza Saudi Arabia na katika nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.
Al Sheikh ameongeza kuwa, vilevile limefunguliwa faili la kuchunguza makaburi ya umati na watu wa kaumu ya Izadi waliouliwa katika hujuma na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la Sinjar mkoani Nineveh, huko kaskazini mwa Iraq.
Baada ya kushambulia eneo la Sinjar huko Iraq mwaka 2014, kundi la kigaidi la Daesh liliwaua kwa halaiki wanaume wa kaumu ya Izadi na kuwateka nyara maelfu ya wanawake wao waliokuwa wakitumiwa kama watumwa wa ngono au wanauzwa kama watumwa. Baadhi ya wanawake hao walikombolewa na wapiganaji wa kujitolea wa al Hashdu al Shaabi au jeshi la Iraq na wengine wengi hawajulikani waliko.
Kundi la kigaidi la Daesh lilianzishwa na kufadhiliwa na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao.