Jasusi aliyesababisha mauaji ya kikatili ya watu 40 Iraq atiwa mbaroni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53211-jasusi_aliyesababisha_mauaji_ya_kikatili_ya_watu_40_iraq_atiwa_mbaroni
Shirika la Ujasusi wa Kijeshi la Iraq limetangaza habari ya kutiwa mbaroni jasusi mmoja wa genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS) mjini Mosul ambaye alisababisha watu 40 kuuliwa kikatili nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 01, 2019 14:03 UTC
  • Jasusi aliyesababisha mauaji ya kikatili ya watu 40 Iraq atiwa mbaroni

Shirika la Ujasusi wa Kijeshi la Iraq limetangaza habari ya kutiwa mbaroni jasusi mmoja wa genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS) mjini Mosul ambaye alisababisha watu 40 kuuliwa kikatili nchini humo.

Shirika la habari la IRNA limenukuu taarifa ya shirika hilo la kijasusi la Iraq ikisema kuwa, kundi moja la makamanda wa operesheni huko Nainawa (Nineveh) wamefanikiwa kumtia mbaroni jasusi mmoja wa genge la Daesh magharibi mwa mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jasusi huyo alikuwa akifanya ujasusi kuhusu familia za watu waliokuwa wanakimbia dhulma na ukatili wa Daesh na kwamba uchochezi wake wa kijasusi ulipelekea kutekwa na kuuliwa kinyama watu 40 wa familia tofauti na genge hilo la ukufurishaji.

Abubakar al Baghdadi, kiongozi wa genge la kigaidi la na ukufurishaji la Daesh (ISIS)

 

Wakati huo huo maswali mengi yamejitokeza hivi sasa baada ya kiongozi wa Daesh, Abubakar al Baghdad kujitokeza tena baada ya kupotea kwa karibu miaka mitano. Maswali mengi yanaulizwa kuhusu njama za baadaye za madola yaliyolianzisha genge la ISIS hasa Marekani huko Iraq na katika eneo nyeti la Asia Magharibi.

Kiongozi wa Daesh amejitokeza tena wakati huu ambapo wananchi wa Iraq wameongeza mashinikizo yao ya kutaka wanajeshi vamizi wa Marekani watoke nchini mwao. Hivyo maswali mengi yamejitokeza kuhusu malengo ya Marekani na vibaraka wake katika suala zima la kujitokeza tena Abubakar al Baghdad hivi sasa.