Umoja wa Mataifa: Vita vimeirejesha nyuma Yemen miaka 20
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55101-umoja_wa_mataifa_vita_vimeirejesha_nyuma_yemen_miaka_20
Mkurugenzi wa Ustawi wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa vita vya uharibifu huko Yemen vimeirejesha nchi hiyo miaka 20 nyuma katika upande wa ustawi na kupatikana huduma za kielimu na mafunzo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2019 03:49 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Vita vimeirejesha nyuma Yemen miaka 20

Mkurugenzi wa Ustawi wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa vita vya uharibifu huko Yemen vimeirejesha nchi hiyo miaka 20 nyuma katika upande wa ustawi na kupatikana huduma za kielimu na mafunzo.

Akizungumza na shirika la habari la Associated, Achim Steiner ameashiria hali ya kibinadamu huko Yemen na kueleza kuwa uchumi wa Yemen umesambaratika kutokana na vita vinavyoendeshwa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia. Steiner ameongeza kuwa raia mmoja wa Yemen kati ya watatu wa nchi hiyo yupo katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na utapiamlo. 

Utapiamlo; tatizo kuu lililosababishwa na vita huko Yemen
 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameashiria pia kubomolewa shule na kushindwa kwenda shule mamilioni ya watoto kutokana na kuendelea mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudia na kueleza kuwa: Kizazi kikubwa cha watoto wa Yemen wameshindwa kwenda shule kutokana na mashambulizi hayo yanayoongozwa na utawala wa Aal Saud.  

Si hayo tu tu bali uvamizi huo umewasababishia wananchi wa Yemen matatizo kama ya uhaba mkubwa wa chakuna na dawa za matibabu. Utawala wa Aal Saud na waitifaki wake hadi sasa wameshindwa kutimiza malengo yao katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu yaani ya kuwarejesha madarakani vibaraka wao kutokana na muqawama uliodhihirishwa na wananchi wa Yemen.