Sep 08, 2019 02:35 UTC
  • Utawala wa Bahrain wawakamata wanazuoni wa Kishia

Utawala wa kiimla wa Bahrain umewakamata wanazuoni kadhaa wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia katika mwezi huu wa Muharram.

Taarifa zinasema utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umewaita na kuwasaili wanazuoni kadhaa wakiwemo Seyed Jaber al-Shahrakani, Sheikh Mohammad Ali al-Mahfuz, Sheikh Mohammad A’ashur na Sheikh Zoheir al-Khal.

Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu ya Hijria Qamaria. Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengine kote duniani hujumuika katika siku 10 za kwanza za Muharram kuomboleza kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS pamoja na wafuasi wake watiifu.

Maandamano dhidi ya utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrian 

Taarifa zinasema wanazuioni kadhaa tayari wametiwa mbaroni na hadi sasa waliobainika kukamatwa ni Sheikh Menbar al-Ma’atouq na Sheikh Mohammad al-A’ajimi.

Aidha wakuu wa utaala wa Aal Khalifa wamewazuia Waislamu katika maeneo kadhaa kupandisha bendera ambazo hutumika katika maombolezo ya siku 10 za Muharram.

 

Tags