Mfalme wa Saudia amteua mwanae kuwa waziri wa nishati
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55875-mfalme_wa_saudia_amteua_mwanae_kuwa_waziri_wa_nishati
Mfalme wa Saudi Arabia amemfuta kazi waziri wa nishati Khalid Al-Falih na kumteua mwanae kuchukua nafasi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2019 03:16 UTC
  • Mfalme wa Saudia amteua mwanae kuwa waziri wa nishati

Mfalme wa Saudi Arabia amemfuta kazi waziri wa nishati Khalid Al-Falih na kumteua mwanae kuchukua nafasi hiyo.

Taarifa zinasema mfalme Salman Bin Abdul Aziz wa Saudia amemeteua mwanamfalme Abdul Aziz bin Salman bin Abdul Aziz Aal Saudi kuwa waziri wa nishati.

Khalid al-Falih alianza kuhudumu kama waziri wa nishati Mei 2016 na hivi karibuni pia alitimuliwa kama mwenyekiti wa shirika la mafuta la ARAMCO.

Mrithi wa ufalme wa Saudia Mohammad bin Salman

Duru zinadokeza kuwa kumekuwepo na hitilafu kubwa baina ya al Falih na mrithi wa ufalme wa Saudia Mohammad bin Salman kuhusu usimamizi wa shirika la ARAMCO.

Bin Salman amekuwa akitaka kuuza hisa za ARAMCO lakini al Falih anapinga vikali pendekezo hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mohammad bin Salman amekuwa akimtimua kila ambaye anapinga sera zake Saudia na hivyo kuibua mgawanyiko mkubwa katika ufalme huo wa kiimla.