Hamas yalaani nchi za Kiarabu zinazopigania kuwa na uhusiano na Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imezilaani nchi za Kiarabu ambazo zinapigania kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Hamas imesema hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kuwa mwenyeji wa kundi moja kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel ni katika fremu ya sisitizo la baadhi ya tawala za Kiarabu la kutaka kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Msemaji wa Hamas, Hazem Qassem amelaani vikali hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa mwenyeji wa kundi moja la utawala wa Kizayuni ambao unaendelea kufanya hujuma na jinai za kibinadamu dhidi ya taifa la Palestina sambamba na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Wiki hii kundi moja la wanafunzi kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel lilishiriki katika Olimpiadi ya roboti huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Katika siku za hivi karibuni baadhi ya tawala za Kiarabu zimeongeza kasi ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.