"Marekani inachochea maandamano katika nchi za Kiarabu kwa maslahi yake"
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57220-marekani_inachochea_maandamano_katika_nchi_za_kiarabu_kwa_maslahi_yake
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inatumia maandamano yanayoshuhidiwa hivi sasa katika nchi kadhaa za Kiarabu kusukuma ajenda zake, na kuifanya Lebanon ishindwe kujisimamia yenyewe.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Nov 12, 2019 04:41 UTC

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inatumia maandamano yanayoshuhidiwa hivi sasa katika nchi kadhaa za Kiarabu kusukuma ajenda zake, na kuifanya Lebanon ishindwe kujisimamia yenyewe.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo katika hotuba yake kwa wafuasi wake kwa njia ya televisheni katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kuongeza kuwa, "Wamarekani wanatumia fursa ya maandamano yanayoshuhudiwa Lebanon na Iraq kwa ajili ya maslahi yao."

Amesema badala ya Marekani kuzingatia zaidi mahitaji ya kimaisha ya wananchi wanaoandamana kama vile umaskini na ukosefu wa ajira, wao wameshupalia kutaka tu maandamano hayo yaendelee. 

Sayyid Hassan Nasrullah ameeleza bayana kuwa, maandamano yamewaunganisha na kuwafanya wananchi wa Lebanon wawe kitu kimoja wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule, na hivi sasa Walebanon wote wamesimama kidete dhidi ya mafisadi serikalini.

Marekani inachochea ghasia katika maandamano ya Walebanon

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, "Kampeni dhidi ya ufisadi inapaswa kushughulikiwa na Idara ya Mahakama kwa uaminifu na kutoegemea upande wowote na pia kwa kuundwa mkakati wa kurejeshwa fedha zote zilizofujwa. Mahakama ianze na wanachama wa Hizbullah."

Amesema Marekani inafanya kila iwezalo ili kuishinikiza kiuchumi Lebanon. Amefafanua kuwa, "Vikwazo vya Marekani vimefunga njia zote za uchumi kati ya Lebanon na Iraq. Imeendelea kufunga mipaka ya nchi mbili hizi licha ya mwito wa mara kwa mara wa kutakiwa ifunguliwe unaotolewa na Adel Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq."