Bahrain yawahukumu kifo wanaharakati wawili wa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58403-bahrain_yawahukumu_kifo_wanaharakati_wawili_wa_nchi_hiyo
Utawala wa Bahrain umewahukumu kifo wanaharakati wawili wa masuala ya kisiasa wa nchi hiyo.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Jan 09, 2020 04:49 UTC
  • Bahrain yawahukumu kifo wanaharakati wawili wa nchi hiyo

Utawala wa Bahrain umewahukumu kifo wanaharakati wawili wa masuala ya kisiasa wa nchi hiyo.

Jumuiya ya al Wifaq al Islami ya Bahrain imelaani hukumu hiyo ya kimaonyesho iliyotolewa ya mahakama ya Bahrain dhidi ya wanaharakati wawili wa kisiasa na kutangaza kuwa, hukumu hiyo ya kifo ni kielelezo cha udhaifu wa utawala wa ukoo wa al Khalifa na jinsi unavyotumia mabavu na ukandamizaji dhidi ya harakati ya amani ya wananchi wa Bahrain.

Taarifa ya al Wifaq al islami imezitaka jumuiya za kimataifa kutekeleza majukumu yao kuhusiana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika nchini Bahrain.

Jumatato ya jana mahakama kimaonyesho ya Bahrain ilitoa hukumu ya kunpokonywa uraia, adhabu ya kifo au kifungo cha maisha jela dhidi ya wanaharakati hao kwa sababu zisizo na msingi.

Bahrain ilianza kushuhudia harakati za wananchi dhidi ya utawala ulioko madarakani wa Aal Khalifa tangu Februari 14 mwaka 2011 huku ukandamizaji unaofanywa na utawala huo ukizitia hofu na wasiwasi fikra za waliowengi na taasisi za kutetea haki za binadamu ulimwenguni.

Utawala wa ukoo wa al Khalifa unakandamiza raia wa Bahrain

Mwezi Juni mwaka uliopita, utawala wa Aal-Khalifa ulimfutia uraia Sheikh Isa Qassim, mwanazuoni mashuhuri na mkuu wa kimaanawi wa mapinduzi ya watu wa nchi hiyo suala ambalo lilikabiliana na radiamali kali kutoka ndani na nje ya nchi hiyo.

Sheikh Ali Salman Katibu Mkuu wa Jumuiya ya al-Wifaq nchini Bahrain ni shakhsia mwingine ambaye amekuwa akizuiliwa na vyombo vya Aal-Khalifa tangu mwezi Julai mwaka jana kwa tuhuma bandia dhidi yake. Kwa mujibu wa Adel al-Gharif mwanaharakati wa Bahrain, kamatakamata na dhulma zote zinazoshuhudiwa nchini Bahrain, zinasimamiwa kwa ukamilifu na idara ya ujasusi ya Saudia.