Bin Salman azidi kuwakandamiza wakosoaji kutokana na uungaji mkono wa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58856-bin_salman_azidi_kuwakandamiza_wakosoaji_kutokana_na_uungaji_mkono_wa_trump
Mwanaharakati mkosoaji wa Saudia Arabia ameeleza kuwa uungaji mkono wa Rais Donald Trump wa Marekani kwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia unamfanya mrithi huyo wa kiti cha ufame azidi kuwakandamiza waziwazi wale wote wanaoukosoa utawala huo wa Aal Saud.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2020 04:17 UTC
  • Bin Salman azidi kuwakandamiza wakosoaji kutokana na uungaji mkono wa Trump

Mwanaharakati mkosoaji wa Saudia Arabia ameeleza kuwa uungaji mkono wa Rais Donald Trump wa Marekani kwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia unamfanya mrithi huyo wa kiti cha ufame azidi kuwakandamiza waziwazi wale wote wanaoukosoa utawala huo wa Aal Saud.

Ghanim al Masarir al Dosari mkosoaji wa Kisaudia ameeleza kuwa huko nyuma viongozi wa Riyadh walikuwa wakifanya kwa siri vitendo vyao viovu na vichafu lakini katika zama hizi za uongozi wa Muhammad bin Salman wanafanya maovu yao waziwazi bila kificho mbele ya wananchi. 

Al Dosari ameashiria namna alivyoshambuliwa na raia kadhaa wa Kisaudia huko London na kuongeza kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia anawafutilia pakubwa wapinzani walioko nje ya nchi hiyo. Mwanaharakati huyo mkosoaji wa Kisaudia ameendelea kubainisha kuwa alinusurika kuuliwa muda mfupi kabla ya kuuliwa Jamal Khashoggi mwandishi habari na mmoja wa wakosoaji wa utawala wa Aal Saud. 

Mwanaharakati mkosoaji wa Kisaudia, Ghanem al Dosari 

Al Dosari ameashiria pia kwamba utawala wa Aal Saud haukuadhibiwa kwa mauaji ya Khashoggi na kusisitiza kuwa viongozi wa Saudia hawatahukumiwa kamwe kwa jinai chungu nzima wanazofanya madhali kuna watu ndani ya White House wanaowaunga mkono. Vitendo vya kuwakandamiza wapinzani na wakosoaji wa utawala wa Saudi Arabia vimeongezeka sana tangu mwezi Juni mwaka 2017 wakati Muhammad bin Salman alipoanza kukalia kiti cha mrithi wa ufalme wa nchi hiyo. Aidha kutiwa mbaroni wana wafalme kadhaa mwezi Novemba mwaka 2017 na kuuliwa Jamal Khashoggi mwezi Oktoba mwaka uliofuta ni miongoni mwa vitendo hivyo vya ukatili na ukandamizaji vilivyofanywa na Muhammad bin Salman.