Hizbullah ya Iraq yasisitizia tena ulazima wa kulipiza kisasi kwa Marekani
Msemaji wa Harakati ya Hizbullah ya Iraq amesema kuwa, wanamuqawama wa harakati hiyo wanaendelea kulinda haki yao ya kulipizai kisasi cha jinai za Wamarekani katika kuwaua kigaidi makamanda wa muqawama.
Mohammed Mohieh ameyasema hayo sambamba na kutimia siku 40 tangu alipouawa shahidi mjini Iraq Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran IRGC na Abu Mahdi al-Muhandis, Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq. Amesisitiza kuwa iwapo Wamarekani watakwenda kinyume na irada ya taifa la Iraq kwa kuamua kuendeleza uvamizi wao dhidi ya ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu, basi Hizbullah ya Iraq inao uwezo na irada ya kutosha ya kukabiliana na wavamizi hao. Aidha Msemaji wa Harakati ya Hizbullah ya Iraq ametaka kuvunjwa haraka makubaliano ya kistratijia na Marekani kama ambavyo ameitaka serikali mpya ya Iraq kuheshimu haki ya kujitawala nchi hiyo na kutokuwepo wenzo wowote wa kuzidisha au kuendeleza uwepo wa askari wa kigeni au kuanzishwa kambi nyingine mpya za kijeshi nchini humo na badala yake itekeleze azimio la bunge la nchi hiyo linalotaka kutimuliwa askari hao vamizi wa Kimarekani.
Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran IRGC na liyekuwa amewasili Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo na kupokelewa na Abu Mahdi al-Muhandis, Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq waliuawa shahidi tarehe 3 Januari karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Kufuatia jinai hiyo ya kinyama tarehe 8 Januari jeshi la IRGC la Iran lilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain Assad na kusababisha hasara kubwa za mali na roho.