Wabunge wa Ufaransa waunga mkono kuwekewa vikwazo vya kimataifa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62235-wabunge_wa_ufaransa_waunga_mkono_kuwekewa_vikwazo_vya_kimataifa_israel
Wabunge wa Ufaransa wameunga mkono kuwekewa vikwazo vya kimataifa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2020 07:53 UTC
  • Wabunge wa Ufaransa waunga mkono kuwekewa vikwazo vya kimataifa Israel

Wabunge wa Ufaransa wameunga mkono kuwekewa vikwazo vya kimataifa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Gazeti la Le Figaro la Ufaransa limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, zaidi ya wabunge mia moja wa Ufaransa wamehimiza kutambuliwa rasmi nchi ya Palestina na kulaaniwa njama za utawala wa Kizayuni za kutaka kuteka ardhi zaidi za Wapalestina. Wabunge huo aidha wameitaka jamii ya kimataifa kuuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wawakilishi hao wa Bunge la Taifa na la Senate la Ufaransa vile vile wamesema, mpango wa utawala wa Kizayuni wa kuteka ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni hatari sana na wamezitaka nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya EU kuitambua rasmi nchi ya Palestina na kama umoja huo utashindwa kufanya hivyo, basi Ufaransa pekee iitambue ifanye hivyo. 

Benjamin Netanyahu akionesha namna ya kutekeleza njama za kupora ardhi zaidi za Wapalestina

 

Tarehe 9 mwezi huu wa Julai pia, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na kumtaka aachane na mpango huo wa kupora ardhi zaidi za Wapalestina. Nchi za Ujerumani na Uingerezanazo zimetoa mwito huo huo kwa utawala pandikizi wa Israel.

Waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni aliahidi kuanza kutekeleza njama za kupora ardhi zaidi za Wapalestina za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuanzia tarehe Mosi mwezi huu wa Julai, lakini wimbi kubwa la upinzani wa dunia nzima limemtia hofu na kumlazimisha asitishe mpango huo.